Skip to content
Kisii University
Back to News

Chuo Kikuu cha Kisii yahidimisha Siku ya Kiswahili Duniani

Posted on Jul 09,2025 by kisii-university
ARTS & CULTURE
...

Chuo Kikuu cha Kisii kwa kushirikiana na Wizara ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Urithi pamoja na Shirika la UNESCO, kiliandaa kongamano la kitaaluma kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani leo tarehe 7 Julai 2025. Kongamano hilo lilifanyika katika majengo ya chuo kikuu na liliwaleta pamoja wataalamu wa lugha, wanazuoni, wanafunzi, wanahabari na wadau mbalimbali wa Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi. Kongamano hili lilidhihirisha dhamira ya Chuo Kikuu cha Kisii ya kuendeleza lugha ya Kiswahili kama nguzo muhimu ya maarifa, utambulisho na mshikamano wa kimataifa.


Kisii University Support
close
send